YALETAYO FURAHA NA AMANI KATIKA NDOA
Kutiana Moyo na Kutakiana Mema
Jifunze kumtia moyo na kumtakia mema mwenzako. Mpenzi wako anapofanya vizuri mpongeze iwe mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Kadiri tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi pia.
Kutokuwa na Kiburi na Majivuno
Mtu mwenye kiburi huwa na majivuno kwa kuamini kwamba hakuna kinachoweza kumbabaisha. Daima kila unaloelekezwa hufanyi, badala yake unakuwa mtu katika kupuuzia mambo. Mfano: Unaweza ukawa mmepanga miadi wewe na mwenzi wako mkutane mahali, lakini unaamua kutokwenda bila sababu ya msingi.
Mpo katika maongezi ya faragha, mwenzio anajaribu kukuelewesha katika maeneo ambayo huwa unakosea, lakini badala ya kupokea ukweli, unaamua kunyamaza kimya, kufoka na kumjibu vibata halafu unamkunjia sura kana kwamba anachokwambia si ukweli bali ni uzushi tu.
Tabia hii ukiwa nayo ni rahisi kuachwa kwa sababu hakuna siku ambayo mpenzi wako atakuwa anajisikia faraja kuwa na wewe.
Usafi
Usafi ni jambo muhimu sana katika kujihakikishia tunafurahia mapenzi na kupendana. Usafi wa Mwili na mazingira ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku.
Tusiruhusu harufu za ajabu ajabu iwe ya mwili au mazingira hasa zile zinazoweza kuharibu starehe ya tendo la ndoa. Tujitahidi kuwa wasafi kwa kufanya usafi wa mazingira yanayotuzunguka (ndani na njeya nyumba), kuoga mara kwa mara hasa kabla hatujakutana na wenza wetu, tusafishe sehemu zote ambazo tunahisi zina tabia ya kutoa harufu, tunyoe nywele za kwenye makwapa na sehemu za siri kwani nazo zinachangia kuleta harufu na mba wakati mwingine.
Pia tujitahidi kupaka mafuta au manukato yenye harufu nzuri ili kujenga hali ya mvuto kwa wale wanaotupenda.
Heshima na adabu
Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mwenzi wako kwa hali yoyote na usonyeshe dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo.
Wasichana wanatakiwa kutambua kuwa linapokuja suala la mahusiano ya kimapenzi au ndoa uzuri sio kigezo cha pekee cha kumfanya mwanamke aolewe. Ingekuwa hivyo basi wanawake wote warembo wangekuwa ndani ya ndoa leo hii. Hii Inamaanisha kuwa hata ukiwa mzuri hutakiwi kujisahau ukaona umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.
Unyenyekevu
Unyenyekevu ni mbolea ya mapenzi, kinyume chake ni sumu, ndiyo maana ubishi ni sumu katika uhusiano wa kimapenzi. Changamoto hii, kama ingekuwa inaeleweka vizuri na kuzingatiwa inavyotakiwa, pengine kusingekuwa na watu wanaotengana.
Binadamu tumeumbwa na udhaifu, kwahiyo kukosea siyo vibaya kwa kuwa ni sehemu ya maisha yetu. Pamoja na kulifahamu hilo, lakini wengi wetu huwa hatutaki kukubali ukweli katika yale tunayokuwa tumekosea.
Tunataka tushinde kwa hoja hata kwenye mambo ambayo tunastahili kuwaomba radhi wapenzi wetu. Tabia ya namna hiyo huwaumiza wenzetu moyoni kwa sababu wao huamini wamekosewa, kwahiyo hutarajia angalau kuombwa msamaha.
Fikiria mpenzi wako amekufanyia kosa ambalo wewe unaliona kama ni kubwa, unamuweka chini unaongea naye, lakini mwenzako anakuruka futi hamsini. Hataki kukubali kosa na zaidi anataka mbishane mpaka makoo yawakauke. Embu chukuliwa wewe ndo ungekuwa umefanyiwa hivi na mpenzi wako, ungejisikiaje?
Maumivu ambayo unahisi wewe ungeyapata endapo ungefanyiwa kitendo kama hicho, basi ujue kuwa ndiyo anayopata mwenzako kutokana na tabia yako ya kutotaka kukubali ukweli.
Uvumilivu
Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika. Hakuna mapenzi duniani yanayoweza kushamiri bila ya uvumilivu. Usipokuwa na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtu utamuona hafai na kila siku utakuwa mtu wa kuanzisha mahusiano mapya.
Mahusiano yaliyodumu si kwa kuwa wahusika hawakoseani au makosa wanayokoseana ni madogo sana, hapana. Kila binaadamu ana mapungufu yake. Wote ambao mahusiano yao yamedumu, wanakoseana ila tofauti yake na wengine ni kwamba busara na uvumilivu huwa msingi wa mapenzi yao na ndiyo maana tunaona wanadumu mpaka leo.
Ni binaadamu gani ambaye unaweza kuishi naye mda mrefu na msikoseane? Hakuna binadamu wa aina hiyo.
Mapenzi yasiyo kuwa na uvumilivu ndani yake hayana maisha marefu. Kwa sababu binadamu ni kiumbe dhaifu na wakati wowote anaweza kukosea.
Uaminifu
Hakuna kitu kinauma katika uhusiano wa kimapenzi kama kugundua kuwa yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu, ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kushea mapenzi.
Kamwe usiuumize moyo wa mtu anayekupenda kwa dhati, usimfanye ajute kuwa nawe maishani na usimfanye anung'unike kwa unayomtendea. Unaweza kuona ni ujanja lakini ipo siku utahitaji mapenzi ya kweli kwa mwingine na hutayapata. Laana ya mapenzi ipo. Ukimuumiza mtu ambaye anakupenda kwa dhati, ipo siku nawe utaumizwa tu.
Msamaha
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.
Huruma na Kujali
Ndani ya uhusiano, huruma ni kitu muhimu sana, kwa sababu mtu mwenye anayejali na mwenye huruma kamwe hawezi kumfanyia mwenzake mabaya.
Uhusiano wa kimapenzo wenye kujaliana na kuoneana huruma, hudumu milele na kutenganishwa na kifo. Asiyekuwa na huruma, hufanya jambo lolote bila kujali maumivu ya mwenzake.
Tendo la ndoa
Kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao hasa kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu.
Bila ya tendo la ndoa hakuna ndoa. Lakini pia izingatiwe kuwa kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi, ni lazima ijengwe na kuimarishwa na upendo, kujituma, utundu na ububunifu.
Hivyo ili uweze kumridhisha vyema mwenzi wako ni vyema kwa wana ndoa wakawa waanazungumzia kuhusu tendo la ndoa ili kubaini kama mwenzi wako kama anaridhika katika tendo au la, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda, wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho kinakupandisha mzuka n.k huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo.
Hitimisho
Yapo mambo mengi sana ambayo yakifanywa yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ndoa na kuifanya ndoa hiyo iwe ya amani, upendo na furaha. Lakini haya niliyoyaandika ni baadhi tu na ni mambo ya msingi ambayo kila mwanandoa ambaye anatamani kuwa na ndoa yenye amani, upendo na furaha anapaswa kuayafuata kwa sababu hapa ndipo msingi wa upendo ulipo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Category 1
KUHUSU MIMI
Search This Blog
Blog Archive
-
▼
2018
(16)
-
▼
January
(15)
- SHEREHE
- UBUYU UNAUZWA
- YALETAYO FURAHA NA AMANI KATIKA NDOA
- Jee unahisi umeshaanza kumchoka mumueo au mkeo?
- MAMBO 8 YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA
- UMUHIMU WA KUPEANA ZAWADI KATIKA NDOA
- SIRI YA ZAWADI KATIKA MAHUSIANO
- FAMILIA
- UTATUZI
- MIGOGORO
- NDOA ZA KIISLAMU
- AINA ZA NDOA NA HUKUMU ZAKE
- NDOA ZA WATANZANIA
- FURAHA
- ZAWADI
-
▼
January
(15)
Comments
DABII
MTUNZI
Pages
-
Moja ya kitu ambacho kinahitaji kipaumbile katika mahusiano ni zawadi, kwani huwa na maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi....
-
Mwanamke anahitaji alama za upendo kutoka kwa mwanaume. Mwanaume anapompelekea mwanamke (mkewe) zawadi hii hudhihirisha kwamba mwan...
Popular Posts
-
Mwanamke anahitaji alama za upendo kutoka kwa mwanaume. Mwanaume anapompelekea mwanamke (mkewe) zawadi hii hudhihirisha kwamba mwan...
-
Imeandikwa na Shams Elmi (Abu 'Ilmi) Takriban katika maisha ya wanandoa walio wengi kama sio wote, ndoa zao hupitia katika vipindi t...
-
Katika makala hii fupi inshaAllaah tutajaribu kuzitambulisha aina za ndoa na kuweza kuzijua hukumu zake kisheria pamoja na maelezo k...
-
Kutiana Moyo na Kutakiana Mema Jifunze kumtia moyo na kumtakia mema mwenzako. Mpenzi wako anapofanya vizuri mpongeze iwe mbele za watu au...
-
kama tunavyofahamu kuwa familia ni kundi la watu wanaokaa pamoja kama Baba, Mama na watoto ambapo hupelekea kuwepo kwa ukoo mkubwa. Yote hay...
-
ukweli usio pingika ni kwamba ndoa nyingi sana huvunjika kutokana na kukosekana kwa suluhisho bora la kutatua matatizo yanayojitokeza katika...
-
Hizi ni ndoa ambazo zinafata sheria ya kiislamu na maagizo ya mtume wetu Muhammad (s.a.w ambazo hukamilika au hufungwa baada ya kutolewa ma...
-
Ndoa ni ktu cha muhimu sana kinachobadilisha maisha ya watu wawili wanapoamua kuishi kwa pamoja. Pale unaposema , Nakubali. ...
0 comments:
Post a Comment